Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania - VIWAWA

Vijana Tulilinde Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC ili imani yetu isije yumbishwa.

Description: C:\Users\Administrator\Desktop\2025\20250112_215658.jpg

Nawasalimu.

MAUJAJI WA MATUMAINI…………..

Naandika barua hii ya wazi kwa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA).

Kwanza nianze kwa kuwasalimu kwa jina la Kristu……

Lengo la barua hii kwa VIWAWA ni kuwakumbusha wajibu wetu sisi kama vijana wakatoliki kama chama hiki kilivyoanzishwa na padre Joseph Cardin uko Ubeligiji mwaka ya 1924. Na hapa Tanzania VIWAWA ilianza rasmi mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi ikiwa chini ya padre Lucas Gaemperle OFM.

Maana ya VIWAWA

VIWAWA ni chama cha kitume cha vijana Wakatoliki Wafanyakzai ambao wanatumwa na kanisa ili kueneza habari njema ya kwamba Yesu Kristu ndiye njia ya ukweli na uzima kwa vijana wote katika maisha yao ya kila siku. Wafanyakazi- ni vijana wa kiume na wanawake waishio mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio katioka ajira rasmi na zisizo rasmi.

Utume wa VIWAWA

Kumwezesha kijana kuwa Mkristo wa kweli ambaye ana ujasiri wa kurekebisha, kuendeleza na kudumisha taratibu za utamaduni, uchumi, siasa na utaalamu kufuatana na mpango wa Mungu. Nilivutiwa na utume wa VIWAWA ambapo mwaka 2022 nikagombea nafasi ya katibu wa VIWAWA parokia ya Maria Mtakatifu Modeko, mkoani Morogoro. Kwa bahati mbaya uongozi wetu ulidumu kwa muda wa wiki mbili kabla baba paroko kuuvunija uongozi kwailionekana kulitokea dosari katika mchakato mzima wa uchaguzi. Baadae uchaguzi uliitishwa tena lakini siku hiyo nilikuwa na majukumu mengine ya kiroho katika kanisa jirani nikiwa kama msimamizi wa ITIFAKI, nililazimika kuongoza mapokezi ya mheshimiwa Januari Makamba na mheshimiwa Maryprisca ambao walikuwa wageni katika harambee ya kumalizia ujenzi wa kanisa katoliki la Mtakatifu Agnes Area Six, Tungi Morogoro.

Sidhani kama kanisa linaweza kutuzuia vijana kwenda mitandaoni kuilinda imani yetu kwa wote wanaotumia ukimya wetu kulidharirisha kanisa katoliki la mitume Tanzania.

Kanisa ni Watu na watu ni Kanisa.

Leo hii Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeamua kusimamia misinga ya kanisa na watu, hii ni misingi iliyojengwa toka zamani sana na ata Oktoba 16, 1970 mwalimu Nyerere alipokuwa rais wa Jamhuri wa Tanzania alitembelea shirika la wamishionari wanawake wa Maryknoll huko New York Marekani. Katika ziara hii mwalimu alitilia jukumu la kanisa katika jamii (soma kitabu cha Man and Development, p. 48) Alisema Umasikini sio tatizo halisi katika dunia ya sasa. Kwakuwa tuna maarifa na maliasili ambazo zinaweza kutoondoa kwenye umasikini. Tatizo halisi ni – vitu ambavyo vinapelekea taabu, vita, na chuki kati ya wanadamu ni tofauti kati ya aliye nacho na siyenacho. Tunaweza kuangalia tofauti hizi kwenye mitazamo miwili: kwenye ngazi ya taifa kuna watu wachache wanaomiliki utajiri mkubwa na utajiri huo unawapa nguvu ya kufanya maamuzi wakati maamuzi hayo yakiwaacha wengi wakiwa waathirika wa maamuzi hayo. Ingawa ata kwenye nchi kubwa kama Marekani unaweza kuuona mgawanyiko huu. Katika nchi kama India, Ureno, or Brazil, mgawanyiko huu kwa wachache wenye nacho na wengi walio masikini ni kashfa kubwa.

Alisisitiza ukweli na undani wa tatizo hili ni kwamba wale wachache wenye utajiri mkubwa wanakuwa na nguvu ya kuamua chochote ata kama hakina maslahi kwa walio masikini.

Mwalimu Nyerere aliliomba kanisa katoliki kutambua mahitaji ya mabadiliko ya kijamii, na kuwa mstari wa mbele kwenye hili. Anaendelea kusema kanisa lazima kushirikiana na wale wote walioanza safari ya kupambania mabadiriko hayo, alisema kwa kufanya hivyo kanisa katoliki litajitambulisha kuwa uhalisia wake katika dunia ya sasa. Kwa lengo la kuwa kanisa ni watu – utu wao na haki ya kuendeleza uhuru wao.

Taasisi zote duniani zimeanzishwa kwa lengo la kuwahudumia wanadamu, likiwemo kanisa katoliki limeanzishwa kuwahudumia na taasisi zake za kanisa kupitia wahumini wake ambao watakuwa mstari wa mbele kushambulia shirika, au uchumi, jamii, au muundo wa kisiasa ambao unakandamiza haki ya mwanadamu, unaowanyima haki na nguvu ya kuishi kama watoto wa Mungu.

Description: C:\Users\Administrator\Desktop\2025\FATHER KITIMA.jpg

Kanisa Katoliki Tanzania.

Kanisa katoliki Tanzania linaheshimu na kutambua mamlaka zote za dola Tanzania kama yalivyo makanisa yote katoliki duniani yanatambu na yataendelea kutambua mamlaka zilizopo katika nchi hizo. Kanisa linalinda na kuendelea kulinda amani iliyopo kwasasa nchini. Lakini kupitia Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania, kanisa limeendelea kulinda misingi yake ya kanisa na ambayo mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyapigani wakati wakati wote wa uhai wake. Mwalimu Nyerere aliona umuhimu wa kanisa katika harakati za ukombozi wa kusini mwa jangwa la Sahara, Kanisa linaendelea kuishauri serikali kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mkataba wa DP World, ulinzi, usalama na haki ya kuishi ya watanzania, uhuru wa kuongea na democrasia.

Hii ndio misingi ya kanisa Katoliki, unaweza kuyaona haya kwenye hotuba mbalimbali alizokuwa akizitoa muhasisi wa taifa hili mwalimu Nyerere. Limekuwa likisimamia haya kwa maslahi mapana ya taifa letu na likiwa na imani kuwa wafaidika watakuwa watanzania kati yao ni waumini wa kanisa katoliki Tanzania. Lakini jitihada hizi za kanisa katoliki za kusimamia misingi ya kanisa imekuwa mwiba kwa watu walafi, walaghai na wapenda chuki na kuanza kuamua kushambulia kanisa katoliki Tanzania, viongozi wa kanisa akiwemo baba Kitima na wengine wengi. Siku za karibuni kumekuwa na makumi ya vijana wakiingia mtandaoni na kudhihaki mfumo wa maisha ya kirho wa mapadri na watawa wetu, wamekuwa wakiwaita majina mabaya mtandaoni, wameanza kuwazushia tuhuma mbalimbali ili kuwarudisha nyuma viongozi wetu wakiroho walioamua kuilinda injili ya kristo.

Wahumini wakatoliki wamejengeka kiimani, na hivyo imani kubwa imekuwa katika kanisa, lakini waumini hawa wakiona wakiona haki yao ya kuongea na kusikilizwa, kuchangua na kuchaguliwa na ongezeko la umasikini miongoni mwa walio wengi na wakati huo kanisa likikaa kimya basi watashindwa kulitofautisha kanisa na kikundi cha watu wachache waliojilimbikizia utajiri mkubwa kwa njia zisizo za halali. Hii itapelekea waamini hawa waache kwenda kanisani, na kwakuwa kanisa ni watu basi huo utakuwa mwisho wa kanisa katoliki. Tukisoma kitabu cha Mathayo 16:18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishindwa. Petro alipewa ufunuo kutoka kwa Yesu Messiah juu ya kanisa hilo. Ni wajibu wa kila mkristu mkatoliki kulilinda kanisa kwa wivu wote.

Description: C:\Users\Administrator\Desktop\2025\YCW.jpg

Nguvu hii inayofanya na vijana mitandaoni kulichafua kanisa katoliki, ni jitihada za watu wenye hira kuhakikisha kanisa katoliki linapungua nguvu au ata kutoweka kabisa. Sisi vijana wakatoliki ni jukumu letu kusimama mstari wa mbele kuilinda imani yetu, kusimama kupingana na yeyote anayekashifu kanisa letu la mitume. Hii ni ahadi ya kila mkristu aliyebatizwa . Tukisoma waroma 6:4, wakolosai 2:12 Mtu anapozamishwa ndani ya maji, anaonyesha kwamba amekufa kuhusiana na maisha aliyokuwa akiishi hapo awali. Anapoinuliwa kutoka kwenye maji, anaonesha kwamba anaanza kuishi upya akiwa Mkristo aliyejiweka wakfu.

Description: C:\Users\Administrator\AppData\Local\Microsoft\Windows\INetCache\Content.Word\Screenshot_20250112_222349_X.JPG

Ni wajibu wa kila mwana VIWAWA kusimama na kulisemea mazuri kanisa letu, kuwasemea viongozi wetu mapabdri, masista na watawa wote wa kanisa katoliki. Tuwaambie kanisa katoliki lilitoa mchango mkubwa sana kuleta amani barani Afrika, lilipigana vikali kuondosha ubaguzi wa rangi kule Afrika ya kuisini kwani wao walikwenda zaidi kuchukua hatua wakati makanisa mengine yalikuwa yakiomba kibali kutoka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi cha nini wafanye na nini wasifanye.

Kutokana na hamasa hii ambayo mwalimu Nyerere aliitoa kwa wamishionari wa Maryknoll New York, basi wamishionari hao wakaongeza nguvu na kufungua taasisi yenye lengo la kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi uko Rhodesia ya Kusini na kaskazini ambazo sasa zinajulikana nchi za Afrika Kusini na Zimbabwe, ofisi hii ilikuwa kwenye mji wa Washington ikiwa na kauli mbiu ya “1970s Justice in The World, Call to Action, and Evangelization in the Modern World” lengo lilikuwa kutatua migogoro ya mataifa mbalimbali kwa kupitia kanisa katoliki. Harakati za kanisa katoliki zilizaa matunda mnamo mwezi Februari 1977 tayari kanisa katoliki lilianzisha mgomo juu ya sera za ubaguzi wa rangi. Kanisa likatanga waafrika weusi wana haki ya kujiunga shule zote za watu weupe zinazomilikiwa na kanisa katoliki vile vile kupata huduma katika hospitali zote za kanisa ambazo zilikuwa zikitoa huduma kwa watu weupe tu (Catholic Defiance of Apartheid Is Stirring South Africa - New York Times, Februari 1977 and www.maryknollogc.org) Haya ni mafanikio makubwa kwa kanisa kusimamia maendeleo ya watu.

Hiki ndio wanachofanya Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania –TEC, baadhi ya watu wameendelea kulishutumu kanisa kujihusisha na maendeleo ya watanzania. Lakini watu hawa pia watakuwa mstari wa mbele kuliambia kanisa lijitokeze kuliombea taifa endapo tu kutakuwa na fujo zitakazo tokana na maelewano mabovu kati ya watawala na watawaliwa.

Unawezaje kuwa mkristo ambaye hauko tayari kuilinda injili? Rai yangu kwa vijana wenzangu wakatoliki kusimama imara kuilinda imani yetu dhini ya wahasimu wanaotumia kila hira kulishusha kanisa katoliki takatifu la mitume.

Na imani wakatoliki wote bila kujari misimamo yao ya kisiasa, nafasi zao za utumishi kwenye vyama vya siasa na serikalini watasimama na mimi kuitetea injili ya bwana kwa kuwapa ulinzi maaskofu wetu kuendelea kusimamia misingi ya imani yetu.

Baada ya kusoma andiko hili basi nakuomba usali Baba yetu mara tatu kama ishara kuwatia nguvu maaskofu wetu……

Shukrani.